Fuata mwongozo huu wa kina ili kukamilisha usajili wako.
Kujisajili kwa SHA kupitia Tovuti ya Afya Yangu tunakupa fursa ya kupata bima ya afya ya umma pamoja na huduma nyingine za Mamlaka ya Afya ya Kijamii (SHA). Fuata mwongozo huu wa kina ili kufanikisha usajili wako.
Mwongozo wa usajili – Hatua kwa hatua:
- Fungua Tovuti ya Afya Yangu kwenye mtandao kwa kuandika Afya Yangu portal, au tembelea: https://afyayangu.go.ke/
- Kwenye tovuti, bofya kitufe cha KUJISAJILI (REGISTER).
- Anza taratibu za usajili.
Dirisha ibukizi litaonekana likiwa na ujumbe:
“JISAJILI kwa Huduma ya Afya kwa Wote (UHC) na SHA kupitia Afya Yangu.”
- Bofya ENDELEA (PROCEED).
- Weka taarifa zako binafsi
- Katika dirisha linalofuata, jaza taarifa zako kama ifuatavyo:
- Chagua raia wa Kenya.
- Weka nambari yako ya simu.
- Weka jina lako la kwanza.
- Weka tena nambari yako ya simu, kisha bofya ENDELEA (PROCEED).
- Thibitisha nambari yako ya simu
- Hakiki nambari yako ya simu ili upokee Nenosiri la Muda Mfupi (OTP).
- Bofya tuma OTP.
- Linda akaunti yako
- Unda PIN ya tarakimu 4.
- Thibitisha PIN yako ya tarakimu 4.
- Bofya ENDELEA (PROCEED). (Sasa umekamilisha 33% ya usajili.)
Endelea na usajili
Bonyeza ENDELEA NA USAJILI.
Weka picha yako
- Katika dirisha lililowekwa, weka picha yako kwa mojawapo ya fomati hizi: JPG, JPEG, au PNG.
- Punguza ukubwa wa picha kama inavyohitajika.
- Bonyeza kitufe cha ✔ kilicho kona ya juu-upande wa kulia wa ukurasa.
Fafanua hali ya kazi
Chagua mojawapo ya chaguzi zifuatazo:
- Umeajiriwa
- Umejiajiri
- Unafadhiliwa
- Kikundi Kilicho Pangiliwa
Fafanua hali ya kiraia
Chagua hali yako ya ndoa kutoka kwenye chaguzi hizi:
- Sijaoa/Sijaolewa
- Nimeoa/Nimeolewa
- Mjane
- Mtalaka
Hali ya ulemavu
- Jibu iwapo wewe ni mtu unayeishi na ulemavu au la.
Endelea kwenye sehemu inayofuata
Bonyeza ENDELEA. (Sasa umekamilisha 66% ya usajili.)
- Toa Taarifa zaidi za mawasiliano
- Ongeza namba mbadala ya simu.
- Ongeza anwani yako ya barua pepe.
- Fafanua anwani yako
Ongeza anwani yako ya makazi ya Sasa kwa kuchagua mojawapo ya zifuatazo:
- Ndani ya Kenya
- Nje ya Kenya
Chagua kaunti, kisha kaunti ndogo, na hatimaye wadi unakoishi.
Kagua na kuthibitisha taarifa zako
- Soma kwa makini taarifa zote ulizowasilisha ili kuhakikisha ni sahihi.
- Weka alama ya tiki kwenye kisanduku cha tamko kuthibitisha kuwa taarifa ulizotoa ni sahihi.
Kuwasilisha usajili wako
Bonyeza WASILISHA (SUBMIT).
Baada ya usajili
Baada ya kukamilisha taratibu zote, utaelekezwa kwenye maelezo yako ya SHA.
Maelezo hayo yanajumuisha:
Maelezo kuhusu madai yako.
Taarifa kuhusu bima yako ya afya.
Rekodi ya ziara zako za hivi punde hospitalini na dawa ulizoandikiwa.
Kalenda na orodha ya miadi yako hospitalini.
Hongera!
Umefanikiwa kujisajili kwa SHA kupitia tovuti ya Afya Yangu.
Mchakato mzima unakamilishwa bila malipo!
Sasa unaweza kufurahia huduma za afya kwa wote na huduma za SHA.



