Mwongozo huu unakuonyesha kila hatua hadi kufanikiwa kuongeza na kuthibitisha wanaokutegemea ili wapendwa wako wapate huduma za afya bila usumbufu.
Unaweza kuongeza: Mtoto uliyemzaa, mtoto wa kupangwa (adopted child), na watoto walio chini ya ulezi wako.
Kuongeza wanaokutegemea kwenye maelezo yako ya Mamlaka ya Afya ya Jamii (SHA) ni muhimu ili kuhakikisha familia yako na/au wengine wanaokutegemea wanapata huduma muhimu za afya chini ya bima yako. Mchakato huu umeundwa kuwa rahisi kwa mtumizi, na unakuwezesha kuweka na kusimamia taarifa za wanaokutegemea mtandaoni.
Mwongozo huu unakuonyesha kila hatua, kuanzia kuingia kwenye maelezo yako ya SHA hadi kufanikiwa kuongeza na kuthibitisha wanaokutegemea, ili wewe na wapendwa wako mpate huduma za afya bila usumbufu.
Hatua ya 1: Fungua maelezo yako ya SHA
Tembelea tovuti rasmi ya SHA: https://sha.go.ke/
Ingia kwenye akaunti yako kwa kutumia nambari yako ya Kitambulisho cha Taifa (ID) na nenosiri.
Hatua ya 2: Nenda kwenye sehemu ya wanaokutegemea
Baada ya kuingia, nenda kwenye sehemu ya Maelezo Yangu (My Profile).
Bofya chaguo la Wanaokutegemea(Dependents).
Hatua ya 3: Ongeza anayekutegemea wa kwanza
Bofya kitufe cha kuongeza anayekutegemea
Chagua aina ya uhusiano wa anayekutegemea:
Mume/Mke
Mtoto wako uliyemzaa
Mtoto wa kupangwa (adopted child)
Mtoto aliye chini ya ulezi wako
Hatua ya 4: Weka taarifa ya anayekutegemea
Kwa mume/mke:
Toa uthibitisho wa ndoa (mfano: cheti cha ndoa, hati ya kiapo, au barua kutoka kwa chifu).
Weka nambari ya simu ya mke au mume wako. OTP itatumwa kwa nambari hiyo ili kutoa idhini.
Kwa mtoto uliyemzaa:
Akiwa chini ya miaka 18: weka nambari ya cheti cha kuzaliwa au nambari ya notisi ya kuzaliwa.
Akiwa na miaka 18 au zaidi: weka nambari ya Kitambulisho cha Taifa (ID).
Kwa watoto wa miaka 21 hadi 25: Toa uthibitisho wa kuwa chuoni.
Kwa watoto walio zaidi ya miaka 25: Wanaweza kuongezwa tu ikiwa wana ulemavu na wako chini ya uangalizi wako; vinginevyo, watajiandikisha kivyao.
Kwa Mtoto wa kupangwa: (adopted child)
Toa nyaraka za kuasili kama uthibitisho.
Ikiwa ana zaidi ya miaka 21: toa uthibitisho wa kuwa chuoni.
Kwa Mtoto aliye chini ya ulezi wako (Loco Parentis):
Toa nyaraka za mahakama zinazoonyesha kuwa wewe ni mlezi halali.
Fuata masharti ya umri kama yalivyo kwa mtoto uliyemzaa.
Hatua ya 5: Pakia nyaraka za uthibitisho
Pakia nyaraka zinazohitajika kama: vyeti vya kuzaliwa, nyaraka za kupangwa (adoption papers), au vyeti vya ndoa, kulingana na anayekutegemea.
Hatua ya 6: Thibitisha na hifadhi
Kagua taarifa ulizoweka ili kuhakikisha ni sahihi.
Bofya Hifadhi (Save) kuwasilisha taarifa za anayekutegemea.
Ujumbe wa uthibitisho utaonekana kuonyesha kuwa mchakato wa kumuongeza anayekutegemea umefanikishwa.
Hatua ya 7: Mchakato wa uhakiki
Taarifa za anayekutegemea zitafanyiwa uhakiki na SHA.
Utapokea ujumbe baada ya mchakato wa uhakiki kufanikishwa.
Taarifa za ziada
Unaweza kuwasimamia wanaokutegemea kwa kuwaongeza au kuwaondoa inapohitajika kupitia sehemu ya wanaokutegemea (Dependents) kwenye maelezo yako.
Hakikisha taarifa zote unazotoa ni sahihi ili kuzuia kucheleweshwa kwa mchakato wa uhakiki.
Kwa kufuata kwa makini hatua zilizobainishwa katika mwongozo huu, unaweza kuboresha maelezo yako kwa urahisi na kuwasimamia wanaokutegemea.
Kumbuka kukagua tena taarifa zote na kupakia nyaraka zinazohitajika ili kuzuia kuchelewesha mchakato wa uhakiki. Kwa usaidizi au maelekezo zaidi, tembelea tovuti ya SHA au wasiliana na timu yao ya usaidizi. Kwa taarifa zaidi, tembelea tovuti rasmi ya SHA: https://sha.go.ke/.



